Benjamin Mkapa yadhamiria kufuta sifuri matokeo kidato cha nne, sita
Mtanzania
by Mtanzania Digital
9h ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa inajivunia kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma kwa mitihani ya kidato cha nne na sita huku ikidhamiria kufuta daraja sifuri. Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1998 ina wanafunzi 1,669 wakiwemo 148 wenye ulemavu wa viungo, ualbino, wasioona na viziwi. Akizungumza wakati wa mahafali ya 24 ya kidato cha sita Mkuu wa shule hiyo, Joseph Deo, amesema maendeleo ya kitaaluma ni mazuri kwani katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023 ilifanikiwa kupata wanafunzi 117 wenye ufaulu wa daraja la kwanza. Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamin Mka ..read more
Visit website
Mifumo ya kidijitali Brela yachochea maendeleo ya viwanda, biashara
Mtanzania
by Mtanzania Digital
9h ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Mifumo ya kidijitali inayotumiwa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) imetajwa kuleta mabadiliko ya ongezeko la matumizi ya Tehama katika huduma mbalimbali zinazotolewa na wakala huo. Kuna Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS) ambao ni maalumu kwa ajili ya kuomba taarifa rasmi za kampuni na majina ya biashara, kupata cheti cha usajili wa kiwanda au leseni ya kiwanda, mfumo wa kielektroniki wa utoaji leseni za biashara na ule wa utoaji taarifa za taratibu za biashara za kimataifa. Wakizungumza Aprili 23,2024 kwenye maonesho ya taasisi za Muun ..read more
Visit website
PPRA yasaini mkataba wa makubaliano na UNDP kuongeza ufanisi
Mtanzania
by Mtanzania Digital
9h ago
Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imesaini mkataba wa makubaliano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 17 (zaidi ya Sh bilioni 40) unaolenga kuiwezesha mamlaka hiyo kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 24, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa PPRA makao makuu jijini Dodoma kati ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Eliakim Maswi na Mwakilishi Mkazi wa UNDP – Tanzania, Shikegi Komatsubara. Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi M ..read more
Visit website
Mchengerwa aagiza kukomeshwa migogoro ya Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi
Mtanzania
by Mtanzania Digital
15h ago
Na Safina Sarwatt, Zanzibar Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo matatu kwa viongozi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM) ikiwemo kuondoa migogoro kati ya wenyeviti wa halmashauri na wakurugenzi wao. Amesema migogoro hiyo inachelewesha maendeleo ya wananchi, na wakati mwingine inamlazimisha Rais aweze kuwatenganisha kwa kumuhamisha mkurugenzi ili kuleta utulivu kwenye halmashauri husika. Waziri wa Mchengerwa ametoa maagizo hayo wakati anafungua Mkutano Mkuu wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyi ..read more
Visit website
Serikali kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
Mtanzania
by Mtanzania Digital
15h ago
*Majiko banifu kusambazwa Kaya za Vijiji na Vijiji-Miji *Wazalishaji wa mkaa mbadala kupewa ruzuku Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema kuwa katika mwaka 2024/25 Serikali itaendelea kutekeleza hatua madhubuti za kuimarisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini. Amesema hayo leo Aprili 24, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2024/25 “Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka ..read more
Visit website
Dk. Biteko: Asilimia 96.37 ya vijiji nchini vimeunganishwa na umeme
Mtanzania
by Mtanzania Digital
15h ago
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Serikali imesema hadi kufikia Mwezi, Machi 2024 jumla ya vijiji 11,837 sawa na asilimia 96.37 ya vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara vilikuwa vimeunganishiwa huduma ya umeme. Hayo yamesema na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko Bungeni, leo Aprili 24, 2024, jijini Dodoma wakati akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2024/2025. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko. Aidha, Dk. Biteko amesema katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa Wananchi vijijini, jumla ya taasisi 63,509 zin ..read more
Visit website
NMB yavifikia vijiji 1,000 nchini ambavyo havikuwa na huduma za kifedha
Mtanzania
by Mtanzania Digital
1d ago
*Yajivunia kuwekeza katika teknolojia na mifumo bora Na Safina Sarwatt, Zanzibar Vijiji zaidi ya 1,000 ambavyo havijafikiwa na huduma za kibenki zimefanikiwa kupata huduma baada ya Benki ya NMB kupeleka huduma za kifedha. Akizugumza katika mkutano wa 38 wa ALAT Taifa uliofanyika Visiwani Zanzibar Aprili 23,2024 Afisa Mtendaji Mkuu benki ya NMB, Ruth Zaipuna amesema lengo ni kufungua akanti milioni 1.5. “Kwa upande wa matawi ya benki yetu ya NMB, takribani tupo katika kila wilaya kwa asilimia 99, na kwa zile halmashauri chache ambazo nazo tunaendelea kuzifanyia kazi kuhakikisha kwamba tunafiki ..read more
Visit website
Hakielimu yatoa rai Serikalini kuhusu bajeti ya elimu 2024/2025
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Esther Mnyika Mtanzania Digital Taasisi ya Hakielimu nchini imetoa rai kwa Serikali kutenga bajeti ya kutosha 2024/2025 katika sekta ya elimu ili kuwezesha kushabihisha bajeti hiyo na malengo ya Dira ya Taifa ya maendeleo katika elimu lakini pia kuanza kwa utekelezaji wa mitaala na sera mpya ya elimu ya mwaka 2023. Akizungumza leo Aprili 23,2024 na waandishi wa Habarijijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hakielimu Dk. John Kalage amesema Serikali imefanya jitihada kubwa za kuleta mabadiliko na uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu. “Pamoja na Serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika ..read more
Visit website
Rais Samia kufanyiwa maombi maalum
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital Kanisa la Uamsho na Matengenezo ya Kiroho, limeandaa kongamano la maombi maalum ya kuliombea Taifa pamoja na  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yatakayofanyika Aprili 28,2024 kwenye viwanja vya Suma JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa  habari leo Aprili 23,2024, jijini, Kiongozi wa kanisa hilo, Mwalimu Augustine  Tengwa amesema Mungu  ndiye aliyemsemesha juu ya maombi hayo kutokana na agano lake kwa Tanzania. “Tangu mwezi wa kwanza aliponiambia Mungu, sikusema. Mungu amenisemasha mambo ambayo yatabeba ajenda ya siku h ..read more
Visit website
Dk. Mpango awataka Watanzania kuuombea Muungano wakizingatia falsafa za 4R
Mtanzania
by Mtanzania Digital
3d ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital-Dodoma Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango amewataka Watanzania kujivunia miaka 60 ya Muungano na kuuombea uendelee kudumu huku wakizingatia falsafa za 4R yaani maridhiano, ustahamilivu, mageuzi na kujenga upya. Akizungumza Aprili 22,2024 wakati wa maombi na dua ya kuliombea taifa yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma, amesema ni baraka kwa taifa kufikia umri huo kwa sababu yako mataifa yaliyojaribu kuungana lakini hayakufanikiwa. “Mengine yaliungana lakini muungano haukudumu, muungano wetu umekuwa tofauti na kudumu kwa zaidi ya nusu karne. Hatu ..read more
Visit website

Follow Mtanzania on FeedSpot

Continue with Google
Continue with Apple
OR