Muonekano mpya Wa Santiago bernabeu 2022
ALVIN HABARI
by Eric C
4y ago
KWANINI REAL MADRID WAMEHAMA SANTIAGO BERNABEU?!. . Kama umegundua siku za hivi karibuni tangu baada ya Corona michezo ya Real Madrid ya nyumbani imekua ikichezwa katika uwanja wa Estadio Alfredo Di Stefano na sio Santiago Bernabeu kama ilivyozoeleka. . Kumeelezwa sababu nyingi na wengi wakiamini kuzuiwa mashabiki kuingia uwanja kuliwafanya Madrid kuacha kuutumia Bernabeu kuepuka gharama za matengenezo kila baada ya mechi,na wakaona labda kutumia Di Stefano itawasaidia katika gharama. . Lakini ukweli ni kwamba Bernabeu upo katika matengenezo na maboresho makubwa ambayo yatachukua muda,taarifa ..read more
Visit website
Dalili Na Tiba Ya Mfadhaiko (DEPRESSION)
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Dalili Na Tiba Ya Mfadhaiko (DEPRESSION)   Maana Ya Mfadhaiko Wa Akili (Depression) Kila mmoja wetu ameshapata kuwa na huzuni wakati fulani, ni kitu cha kawaida kinachotokea wakati umepotelewa na kitu, kutokana na mihangaiko ya maisha au kutokana na kudharauiliwa. Huzuni ikizidi na ikienda kwa siku nyingi mfululizo (wiki mbili au zaidi) na ikiambatana na hali ya kujiona kuwa si wa thamani tena, kwamba ni mtu usiye na msaada wo wote – basi hii inaweza kuwa ni zaidi ya huzuni. Unaweza kuwa umepata tatizo la kiafya – mfadhaiko, ugonjwa ambao kwa bahati nzuri una tiba ..read more
Visit website
Ni Nini Maana Ya Panic Attack? Utakabiliana Vipi Na Panic Attack?
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Ni Nini Maana Ya Panic Attack? Utakabiliana Vipi Na Panic Attack? “Ghafla nilisikia wimbi la hofu likitambaa mwilini bila sababu yo yote ile. Moyo wangu ulienda kasi sana, kifua kiliuma na ikawa inazidi kuwa ngumu zaidi kupumua. Nilifikiri kuwa muda wangu wa kufa ulikuwa umewadia.” Hii ni mfano wa sentensi inayotoka kinywani mwa mtu mwenye tatizo la panic attack. Panic attack inaweza kuelezewa kuwa ni kipindi kifupi cha mtu kukamatwa na hofu kubwa na wasiwasi vinavyokuja ghafla. Moyo ghafla unakwenda mbio na unashindwa kupumua. Unaweza pia kufikiria unakufa au unapata wazimu. Panic attacks ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 14
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Kamanda akanyamaza na kututazama. Kikapita kimya kifupi kabla ya kukitanzua kimya hicho. “Sasa andikisha maelezo yake, yatawekwa kwenye faili la marehemu pamoja na maelezo yenu nyote” Kamanda akamwambia Inspekta na kunigeukia mimi. “Wewe utatupeleka katika hilo eneo, tutachukua mpiga picha” akaniambia. Wakati Inspekta anachukua maelezo ya yule mwananchi, kamanda wa polisi na afisa upelelezi walitoka nje ya kituo wakakikagua tena kiwiliwili cha Sajenti Erick kabla ya kuamuru kipelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi. Baada ya hapo aliitwa mpiga picha wa polisi. Dakika chache baadaye kamanda wa p ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 12
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Sote tukasimama. Kila polisi akachukua bunduki yake. Tulishindwa hata kujibu, tukawa tunatazamana. “Vipi jamani, mbona mmelala hapa” Inspekta Amour akatuuliza tena. Polisi mmoja akaeleza kilichotutokea. Polisi hao waliokuja wakashangaa. Waliusogelea mwili wa Sajenti Erick na kuutazama. “Huyu ndiye Sajenti Erick” Amour akasema baada ya kuutazama mwili huo. Akaongeza. “Sasa nini kilitokea?” “Ni miujiza mitupu” nilijibu mimi. “Hiyo nyumba imetowekaje?” “Hatujui. Muda huu tunazinduka tunaona nyumba haipo” “Ilikuwa kwa wapi” “Sisi tulikuwa uani mwa hiyo nyumba. Lile gari tulilokuja nalo lilikuwa m ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 13
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Baada ya kumaliza maelezo yake ambayo yaliwashangaza maafisa hao, kamanda wa polisi akataka na mimi nieleze kilichotokea. “Kwanza ulifikaje katika eneo hilo na ulikuwa na Sajenti Erick au ulikuwa peke yako?” akaniuliza. “Nilikwenda peke yangu” nilimjibu. “Kufuata nini?” Niliona kama nitauma uma maneno nitajikuta nikiwekwa ndani, jambo la msingi ni kueleza ukweli wote. “Kuna msichana niliwasiliana naye kwenye simu akataka nimfuate katika eneo hilo” “Ni nani?” “Wakati tunawasiliana nilikuwa simjui lakini baadaye niligundua alikuwa ni yule msichana ambaye mama yake tulimshitaki kwa kukutwa na ke ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 10
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Maimuna alikuwa ameshika ule upanga wake akiangaza macho yake huku na huku. Sikuweza tena kusubiri, nikatoka mbio. Nilielekea upande ule lilikoelekea gari la polisi. Wakaniona! “Si yule!” niliisikia sauti ya Maimuna. “Twende tumfuate” Sauti ya kiume nayo ikasikika. Niliendelea kukimbia. Kila nilipopiga hatua tatu nilitazama nyuma. Niliwaona wananifuata. Hawakuwa wakikimbia lakini walikuwa wanakuja kwa haraka. Kwa mbali nikaona mwanga wa gari linalokuja. Nikazidi kukimbia. Niliona nikimbie nikiwa katikati ya barabara ili watu waliomo ndani ya gari hilo waweze kuniona. Nikajitokeza katikati ya ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 11
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Mwili na kichwa vimeondolewa. Nafikiri vimezikwa uani” nikaongezea maelezo. “Tumekuta makaburi uani!” Polisi mwingine akasema. “”Kwenye hivi vyumba vingine hamkukuta watu?” Koplo akauliza. “Hakuna mtu humu ndani. Hii nyumba iko tupu” “Hebu twendeni tukayaone hayo makaburi” Tukaenda uani. Lile kaburi nililoliona likichimbwa na yule mwanamke lilikuwa limefukiwa. Pembeni yake kulichimbwa kaburi jingine lililokuwa wazi. Shepe lilikuwa limeachwa kwenye chuguu ya mchanga. “Hili kaburi lililofukiwa ndilo nililokuta linachimbwa. Bila shaka mwili wa Sajenti Erick umezikwa hapa” nikawambia wenzangu. “T ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 08
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Leo nimekwisha!” nikajiambia. Nilikuwa sina pa kukimbilia. Lakini nilikwishatambua kila kitu. Sikujua niliwezaje kuwasiliana na yule msichana hadi nikafika katika nyumba ile ya mauti! Kusema kweli nilijipeleka mwenyewe! Kwa vyovyote vile, nilijiambia, nyumba ile haikuwa ya binaadamu wa kawaida. Yule bibi alikuwa jini! Na kama alikuwa jini, niliendelea kujiambia, sitaweza kunusurika mle ndani. Licha ya kutoka pale uani, yule bibi hakushituka. Aliendelea kuchimba lile shimo kwa bidii. Hakuna binaadamu yeyote anayekubali kufa kirahisi, nikageuka haraka na kurudi nilikotoka. Wakati nafika kwenye ..read more
Visit website
Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 09
ALVIN HABARI
by ALVIN HABARI
4y ago
Nikajiambia yeye ndiye aliyestahili adhabu aliyoipata lakini mimi nilikuwa naonewa tu. Nikaapa kimoyomoyo kama nitasalimika sitarudia tena kushirikiana na polisi wasio waaminifu. Kwa vile nilikuwa hoi, nikaanguka chini na kupotewa na fahamu. Nikiwa sijielewi niliota nainuliwa na mtu aliyenikuta nimeanguka. “Mbona umelala hapa?” akaniuliza. “Nlinguka nilikuwa nakimbia” nikamjibu. “Oh pole sana. Ulikuwa unakimbia nini?” Nikamueleza ule mkasa ulionitokea. “Kwani wewe ulikuwa hujui kama yule bibi na mwanawe Maimuna ni majini?” “Nilikuwa sijui. Kumbe majini wanaishi na binaadamu?” “Ndio, wanaishi ..read more
Visit website

Follow ALVIN HABARI on FeedSpot

Continue with Google
Continue with Apple
OR