Wanyamapori wakali wametufanya tuhame hifadhini -Wananchi ngorongoro
Mtanzania
by Mtanzania Digital
4h ago
Na Mwandishi wetu Baadhi ya wananchi wanaoishi katika Kijiji cha Endulen ndani ya Tarafa ya Ngorongoro wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kuwahamisha kwa hiyari kutoka kijijini hapo kutokana na kusumbuliwa na changamoto ya Wanyama pori wakali. Wakizungumza katika zoezi la uelimishaji, uhamasishaji na uandikishaji baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa kasi ya ongezeko la wanyama wakali na waharibifu kama fisi, chui, Nyati, simba na tembo imewafanya washindwe kufanya shughuli zao za maendeleo na hivyo kuamua kuondoka kuelekea Msomera na maeneo mengine. Wamesema hawaoni sababu ya kuen ..read more
Visit website
MIAKA 60 YA MUUNGANO: Rais Samia ahimiza falsafa ya 4R kuuenzi
Mtanzania
by Mtanzania Digital
6h ago
Nora Damian na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili muungano uendelee kudumu Watanzania hawana budi kuitekeleza falsafa ya maridhiano, kuvumiliana, mageuzi na kujenga nchi. Amesema kutekelezwa kwa falsafa hizo kutajenga amani na utulivu wa kudumu nchini na kuleta maendeleo endelevu. Akizungumza leo Aprili 26,2024 wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, amesema Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume wamejenga taifa huru, madhubuti na lenye matumaini hivyo, zawadi pekee wanayopaswa ..read more
Visit website
OSHA yatoa mafunzo kwa wajasiriamali 250 Arusha
Mtanzania
by Mtanzania Digital
6h ago
Na Mwandishi Wetu, MtanzanianDigital Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kitakachofanyika Aprili 28 OSHA imeendelea na kampeni ya uhamasishaji wa uwepo wa mazingira salama katika maeneo ya kazi ambapo takribani wajasiriamali 250 wamepatiwa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi mkkoani Arusha. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa pamoja na AICC Club jijini Arusha yamelenga kuwajengea wajasiriamali hao uelewa juu ya masuala mbalimbali ikiwemo Sheria na Miongozo ya usalama na afya mahali pa kazi, utambuzi wa vihatarishi vinavyowakabi ..read more
Visit website
TCRA yatoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mara kuelekea Uchaguzi
Mtanzania
by Mtanzania Digital
12h ago
Na Malima Lubasha, Musoma MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari mkoani Mara juu ya kanuni na Sheria za utoaji Habari hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu. Akizungumza juzi mjini Msoma, Meneja Mawasiliano Kanda ya Ziwa (TCRA), Mhandisi Imelda Salumu amesema mada mbalimbali zilizowasilishwa na wawezeshaji katika warsha iliyofanyika mjini Musoma inalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwa kuwaongezea uelewa ili wasikiuke sheria na maadili ya uandishi habari kuelekea kwenye uchaguzi huo unaotarajwia kufanyika baada ..read more
Visit website
GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto
Mtanzania
by Mtanzania Digital
12h ago
Na Mwandishi Wetu, Arusha Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), imetoa mafunzo maalumu kwa akina mama lishe 50 wa mkoa wa Arusha kwa lengo la kuwaelimisha namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali ya moto. Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk. Kiva Mvungi (kulia) akizungumza na akina mama lishe kuwaeleza namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha. Mbali n ..read more
Visit website
TBL, IFC na COPRA wahimiza mfumo wa kilimo cha mkataba
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
*Lengo ni kuwezesha ufadhili kwa wakulima na ugavi na kusaidia kuiweka Tanzania kama kapu endelevu la chakula kwa ukanda huu *Soko linalofanya kazi vizuri linaweza kuchochea uzalishaji wa kilimo, ukuaji wa uchumi na kutengeneza nafasi za kazi Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) na Mamlaka ya Udhibiti wa nafaka na mazao mengine (COPRA) wamekutana pamoja ili kuwasaidia wakulima wa Tanzania kutambua uwezo wao wa kulisha watu, viwanda na biashara katika ukanda huu kupitia mikataba ya wakulima iliyoimarishwa. Washirika hao walifany ..read more
Visit website
Benjamin Mkapa yadhamiria kufuta sifuri matokeo kidato cha nne, sita
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa inajivunia kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma kwa mitihani ya kidato cha nne na sita huku ikidhamiria kufuta daraja sifuri. Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1998 ina wanafunzi 1,669 wakiwemo 148 wenye ulemavu wa viungo, ualbino, wasioona na viziwi. Akizungumza wakati wa mahafali ya 24 ya kidato cha sita Mkuu wa shule hiyo, Joseph Deo, amesema maendeleo ya kitaaluma ni mazuri kwani katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023 ilifanikiwa kupata wanafunzi 117 wenye ufaulu wa daraja la kwanza. Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamin Mka ..read more
Visit website
Mifumo ya kidijitali Brela yachochea maendeleo ya viwanda, biashara
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Mifumo ya kidijitali inayotumiwa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) imetajwa kuleta mabadiliko ya ongezeko la matumizi ya Tehama katika huduma mbalimbali zinazotolewa na wakala huo. Kuna Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS) ambao ni maalumu kwa ajili ya kuomba taarifa rasmi za kampuni na majina ya biashara, kupata cheti cha usajili wa kiwanda au leseni ya kiwanda, mfumo wa kielektroniki wa utoaji leseni za biashara na ule wa utoaji taarifa za taratibu za biashara za kimataifa. Wakizungumza Aprili 23,2024 kwenye maonesho ya taasisi za Muun ..read more
Visit website
PPRA yasaini mkataba wa makubaliano na UNDP kuongeza ufanisi
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imesaini mkataba wa makubaliano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 17 (zaidi ya Sh bilioni 40) unaolenga kuiwezesha mamlaka hiyo kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 24, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa PPRA makao makuu jijini Dodoma kati ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Eliakim Maswi na Mwakilishi Mkazi wa UNDP – Tanzania, Shikegi Komatsubara. Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi M ..read more
Visit website
Mchengerwa aagiza kukomeshwa migogoro ya Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Safina Sarwatt, Zanzibar Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo matatu kwa viongozi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM) ikiwemo kuondoa migogoro kati ya wenyeviti wa halmashauri na wakurugenzi wao. Amesema migogoro hiyo inachelewesha maendeleo ya wananchi, na wakati mwingine inamlazimisha Rais aweze kuwatenganisha kwa kumuhamisha mkurugenzi ili kuleta utulivu kwenye halmashauri husika. Waziri wa Mchengerwa ametoa maagizo hayo wakati anafungua Mkutano Mkuu wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyi ..read more
Visit website

Follow Mtanzania on FeedSpot

Continue with Google
Continue with Apple
OR