Serikali kuboresha sera ya miliki bunifu
Mtanzania
by Mtanzania Digital
1d ago
Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital Serikali imeweka wazi kuwa inaendelea kuboresha sheria na sera ya miliki bunifu ili kuhakikisha  yanakuwepo mazingira rafiki yenye tija kwa wabunifu na Taifa kwa ujumla. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘ Mwana FA’ wakati alipomuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji katika maadhimisho ya siku ya Miliki Bunifu duniani yalifanyika leo Mei 9,2024, jijini Dar es Salaam. Mwana FA amesema ubunifu ni nyenzo muhimu katika kukuza na kuendeleza biashara, uboreshaji wa sera utaondoa changamoto ..read more
Visit website
Mageuzi makubwa Sekta ya Ardhi yanakuja-Silaa
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema mageuzi makubwa Sekta ya ardhi yanakuja baada ya kushuhudia utiaji saini kati ya Wizara yake na Mtaalamu Mshauri wa Mradi Mkubwa wa Kuimarisha na Kuboresha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) wenye thamani takribani Sh Bilioni 150. Waziri Silaa amebainisha kuwa mradi huo utaongeza uwezo wa wizara wa kuandaa ramani za msingi kwa nchi nzima ambazo licha ya kutumika katika kupanga matumizi ya Ardhi mijini na vijijini, pia zinahitajika kwa matumizi mengine mengi katika ujenzi wa miundombinu ..read more
Visit website
IWPG Global Region 2 met with representatives of Ethiopian EBC Broadcasting Company
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
*Discussed business agreement with Genet Tadesse, CEO of Ethiopian public broadcaster EBC By Our Correspondent On the 30th of last month, a delegation from the International Women’s Peace Group Global Region 2 (IWPG, Global 2 Regional Director Seo-yeon Lee) met at the EBC broadcasting station with EBC Representative Genet Tadesse of Ethiopia, Office Director Molalin, and Reporter Yegawehu. EBC (Ethiopian Broadcasting Corporation) is a public broadcaster that produces and broadcasts a variety of programs to promote Ethiopia’s national development and culture, including domestic and internationa ..read more
Visit website
Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo nchini
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameainisha mpango wa Serikali wa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Mei 9, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Dk. Christine Ishengoma Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga. Ameongeza kwamba, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza zaidi katika utafiti ..read more
Visit website
Jubilee Allianz kuanza kutoa bima ya kilimo
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Katika jitihada za kuwahakikishia usalama wakulima Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz imetangaza kuanza kutoa bima ya mazao kwa wakulima. Mpango huo umetangazwa Mei 9,2024 wakati wa hafla ya kuwatambua mawakala wanaoshirikiana nao na kuwapongeza kwa kufanya vizuri. Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa Jubilee Allianz, Dipankar Acharya, amesema mpango huo unalenga kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini. Meneja wa Mawakala katika Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz, Mary Ndege, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fursa mbalim ..read more
Visit website
TAG wajivunia miaka 85 ya ujenzi wa umoja, amani
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk. Barnabas Mtokambali amesema miaka 85 ya kanisa hilo imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwaunganisha Watanzania na kuchagiza maendeleo katika sekta mbalimbali nchini. Kanisa hilo lililoanzishwa mwaka 1939 Igale jijini Mbeya hadi sasa lina matawi zaidi ya 16,000 nchini huku pia likiwa limefungua makanisa katika nchi za Madagascar, Msumbiji, Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Kenya na Rwanda. Akizungumza Mei 8,2024 na Waandishi wa habari, Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mt ..read more
Visit website
Wanawake Kipunguni njia nyeupe uchaguzi 2024/25
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
Na Nora Damian, Mtanzania Digital “Wanawake tunapewa mbinu nyingi za kushiriki katika uchaguzi, tunapambana vya kutosha lakini tunarudishwa nyuma. Kuna vikwazo vingi tunaomba Serikali itende haki bila kujali mtu anatoka chama gani,” anasema mkazi wa Dar es Salaam, Rehema Mfaume. Rehema ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Serikali ya Mtaa mwaka 2014 ni mfano wa wanawake wengi wenye kiu ya kuwa viongozi katika ngazi za maamuzi lakini wanashindwa kufikia ndoto zao kutokana na vikwazo mbalimbali. Tafiti mbalimbali zinaonyesha ushiriki wa wanawake katika vyombo vya uwakilishi wa wananchi bado ni mdogo ik ..read more
Visit website
CCM Morogoro wamjibu Lissu
Mtanzania
by Mtanzania Digital
2d ago
*Wasema hoja zake hazina mshiko Na Ashura Kazinja, Morogoro Katibu wa Siasa, Uenazi na Mafunzo Mkoa wa Morogoro, Zangina Shanang amejibu hoja tano zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu na wenzake katika mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 30, mwaka huu mkoani Morogoro na kusema kuwa hoja hizo ni za upotoshaji. Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo mkoa wa Morogoro, Zangina Shanang akiongea na Waandishi wa habari mkoani Morogoro. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro Mei 8,2024 Shangina amesema hoja ya Tundu Lissu na wenzake kuhusu uwepo wa Serikali ..read more
Visit website
Kaya 413 zazingirwa na maji Lamadi mkoani Simiyu
Mtanzania
by Mtanzania Digital
5d ago
Na Samwel Mwanga,Busega KAYA 413 zilizoko katika Kata ya Lamadi Wilaya ya Busega mkoani Simiyu zimekosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na hivyo kusababisha kuongezeka kwa kina cha maji kwenye Ziwa Victoria. Nyumba hizo ziko mwambao mwa Ziwa Viktoaria katika kitongoji cha Lamadi, Itongo na Makanisani. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed (wa kwanza kushoto)akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faidha Salum (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye mtumbwi wakikagua makazi ya watu yaliyozingirwa na Maji katika Mji wa Lamadi ulioko wilayani ..read more
Visit website
GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha, Ndejembi awafunda
Mtanzania
by Mtanzania Digital
5d ago
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital ZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa mafunzo maalum ya usalama na afya kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua vihatarishi vya ajali na magonjwa katika shughuli zao za uzalishaji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk. Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha. Mafunzo hayo yaliyotolewa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limi ..read more
Visit website

Follow Mtanzania on FeedSpot

Continue with Google
Continue with Apple
OR